Wakili wa Mahakama Kuu, Ferdinand Makore amesema kwa mujibu wa Katiba baada ya Makamu wa Rais kujiuluzu, Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan atamteua Mtu mwingine mwenye sifa ndani ya siku 14 tangu kujiuzulu kwa Makamu wa Rais kisha jina hilo litapaswa kuthibitishwa na Bunge la Tanzania ili aapishwe kuwa Makamu wa Rais wa Nchi.
Akizungumza Makore amesema “baada ya kiti cha Makamu wa Rais
ndani ya siku 14 Rais atateua Mtu na Mtu huyo itabidi athibitishwe na
Bunge, kwahiyo muda ambao tunao ni siku 14 tangu kujiuzulu kwa Makamu wa
Rais, kwahiyo kama Nchimbi amejiuzulu kwa mujibu wa Ibara ya 149 ibara
ndogo ya pili basi siku 14 zitahesabiwa kuanzia Septemba 04,2026 hilo
ndio jukumu la Rais kutafuta Mtu wa kuziba nafasi ambaye atathibitishwa
na Bunge”
“Mtu huyo ambaye atapelekwa Bungeni kuthibitishwa
anatakiwa awe na sifa za Kiongozi anayefaa kuwa Makamu wa Rais ambazo
zinaainishwa kwenye ibara ya 47 ibara ndogo ya nne, ambapo anatakiwa
kuwa Raia wa Tanzania, atimize umri wa miaka 40 na kuendelea, awe
Mwanachama wa Chama cha Siasa ambacho Mgombea Urais anatumikia, na
anayeweza kuwa na sifa za kugombea ubunge, katika kipindi cha miaka
mitano kabla ya kuteuliwa anatakiwa asiwe ameshtakiwa au kutiwa hatiani
katika makosa ya ukwepaji wa kodi au kudaiwa na Serikali”
“Rais
anaweza kumteua Mbunge kushika madaraka ya Makamu wa Rais kama kiti cha
Makamu wa Rais kipo wazi kisha Mbunge huyo atathibitishwa na Wabunge
wenzake na Jimbo lake litakuwa wazi kwa ajili ya uchaguzi mdogo
kufanyika”
.jpeg)
0 Comments