Mbunge wa
Katoro, Eng. Kija Limbu Ntemi ameitaka Serikali kueleza hatua
zinazohitajika ili Majimbo ya Katoro na Busanda yaweze kupatiwa
Halmashauri akisema majimbo hayo yamekidhi vigezo vya kuwa na
Halmashauri.
Akijibu swali hilo lilioulizwa kwa niaba ya Mbunge
huyo, Bungeni Jijini Dodoma leo Agosti 26, 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe amesema uanzishaji wa
Halmashauri mpya hufuata Sheria za Serikali za Mitaa pamoja na Mwongozo
wa Uanzishwaji wa Maeneo ya Utawala wa mwaka 2025.
Serikali
imesema kusudio la kuanzisha Halmashauri mpya linapaswa kujadiliwa na
kupitishwa na Baraza la Madiwani, Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) na
Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), kabla ya kuwasilishwa na Katibu Tawala
wa Mkoa kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.
Hata
hivyo, Serikali imesema hadi sasa kusudio la Majimbo ya Katoro na
Busanda kupatiwa Halmashauri bado halijawasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu –
TAMISEMI, hivyo Mamlaka zinazohusika zimetakiwa kuendelea na taratibu
kwa kufuata Sheria na Miongozo iliyowekwa.
0 Comments