LISSU KUMALIZA KUJITETEA LEO

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, leo Agosti 26, 2026, anatarajiwa kuhitimisha sehemu ya kwanza ya ushahidi wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili.
 

Leo ni siku ya tatu mfululizo kwa Lissu kuendelea kutoa ushahidi wake mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, ambapo anaendelea kujibu na kuchambua hoja zinazohusiana na mashtaka yanayomkabili.

Katika hatua hiyo, Lissu anatarajiwa kuendelea kuchambua ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka, huku akieleza kile anachodai kuwa ni mapungufu na udhaifu katika ushahidi huo wa upande wa mashtaka.

Baada ya kukamilisha ushahidi wake mkuu, hatua inayofuata katika mwenendo wa kesi hiyo itakuwa ni cross-examination, ambapo Lissu ataulizwa maswali na waendesha mashtaka kuhusu ushahidi alioutoa mahakamani.

Kesi hiyo inasikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu, likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidiwa na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Post a Comment

0 Comments