Na Ally Mandai.
Katika dimba la KMC Complex lililopo Mwenge, jijini Dar es Salaam, pambano la ligi limehitimishwa kwa matokeo makubwa huku Yanga SC ikiandika ushindi mnono wa mabao matano (5-0) dhidi ya JKT Tanzania.
Mchezo huo uliovutia mashabiki wengi ulishuhudia Yanga wakitawala sehemu kubwa ya mchezo kwa kasi, umakini na safu kali ya ushambuliaji iliyowapa mabao hayo muhimu.
Kwa ushindi huo, Yanga wanaendelea kuonyesha ubora wao katika mbio za ligi, huku JKT Tanzania wakilazimika kujipanga upya baada ya kupokea kipigo hicho kizito.
Mshambuliaji Yanga Prince Dube amechukua Tuzo ya mchezaji bora kwenye mchezo wa leo dhidi ya Jkt Tanzania.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Mohamed Hussein,Depu, Mudathir,Dube pamoja na Shekhan Khamisi.
TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804



0 Comments