Na Moshi saidi
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mheshimiwa Edward Mpogolo ametoa maagizo kwa uongozi wa Halmashuri ya Jiji la Dar es salaam Idara ya Elimu kuhakikisha mtoto Ali Kimara mwenye maradhi adimu anatimiza malengo yake ya elimu.
Ametoa maagizo hayo leo hii wakati alipomtembelea kijana huyo nyumbani kwao Upanga kumjulia hali na kumpongeza kwa kumaliza elimu yake ya Msingi na kuweza kuendelea na elimu ya Sekondari kwa muhula huu mpya wa masomo.
Mhe. Mpogolo amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaelekeza kuhakikisha wanawasaidia watu wenye changamoto za ulemavu ili kutumiza malengo yao.
"Nimekuja hapa kukusalimia na kukutakia heri ya mwaka mpya lakini kukupongeza kwa kumaliza elimu ya msingi,naelekeza muhakikishe kijana huyu atimize malengo yake kwa kumuwezesha kusoma kwa kutumia teknolojia akiwa hapahapa nyumbani".Alisema
Kwa upande wake kijana huyo alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kumtembelea na kumuhakikishia kuwa ataoma kwa bidii ili aweze kutimiza lengo lake.
Kijana huyo Ali Kimara anasumbuliwa na maradhi adimu yaliyosababisha alale kitandani kwa muda wa zaidi ya miaka 8 ambapo amemaliza elimu yake ya Msingi amemaliza akisomea kitandani.





0 Comments