Habibu Mchange ameibuka na madai mazito dhidi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwatuhumu kuhusika katika vitendo vya utekaji, mateso na mauaji ya vijana wasio na hatia pamoja na kupanga matukio mbalimbali ya kisiasa tangu mwaka 2011 kwa lengo la kuipotosha jamii na kuichafua taswira ya Serikali.
Kwa mujibu wa Mchange, matukio hayo yanajumuisha vurugu za Arusha, tukio la Morogoro alikofariki mwanahabari Arizona, kifo cha Daud Mwangosi Iringa, madai ya kutekwa na kuteswa kwa Yona Temeke, shambulio la tindikali dhidi ya Musa Tesha, pamoja na madai ya kuteswa kwa Mkurugenzi wa Jambo Media Group Bagamoyo.
Aidha, Mchange ametoa tuhuma za ulaji wa michango ya umma akidai kuwa viongozi wa Chadema wakiongozwa na John Heche waliinisha michango kwa ajili ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, ambapo shilingi milioni 41 zilipatikana lakini kwa umma ikatangazwa milioni 26 pekee.
Amesema shilingi milioni 19 zilitumwa kwa wanaharakati waliopo Nairobi kwa madai ya kuchochea matusi dhidi ya Serikali. Ameongeza pia kuwa michango ya msiba wa mzee Edwin Mtei haijulikani ilipo kwa madai kuwa haikukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu.
Mchange amesisitiza kuwa ana ushahidi wa madai hayo ambao tayari ameuwasilisha katika maeneo mbalimbali, akidai kuwafahamu watu waliodaiwa kuhusika katika baadhi ya matukio hayo.
Akimtaja John Heche na Mnyika, amewataka viongozi wa Chadema kufanya siasa za wazi na za kistaarabu, akisisitiza kuwa amani ya Taifa ni muhimu kuliko maslahi ya vyama vya siasa.
.jpeg)
0 Comments