PACOME KUIKOSA DABI KESHO?,KOCHA WA YANGA ATOA JIBU HILI

Na Ally Mandai.

Kocha wa klabu ya Yanga SC ,Pedro Gonçalves amezungumza na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo wa dabi ya Kariakoo na haya ndio aliyoyazungumza

"Tumeanza maandalizi tangu juzi na leo tunakwenda kumalizia maandalizi hayo, wachezaji wangu wapo tayari na wana morali ya kucheza mechi hii kubwa, kama kila kitu kitaenda sawa nina imani tutakwenda kufanya vizuri kesho" 

"Hii ndiyo derby yangu ya kwanza dhidi ya Simba. Kazi yetu ni kujiandaa kwa ajili ya kushinda kila mechi tunayocheza. Iwe ni dhidi ya Cosmo Politan au Al Ahly, lengo letu siku zote ni ushindi. Ndivyo ilivyo hata kwa mchezo wa kesho; tunalenga kushinda, japokuwa tunatambua kwamba tunakwenda kukutana na mpinzani mwenye uwezo mkubwa.

Simba ni miongoni mwa timu bora nchini Tanzania. Wamewekeza kwa kiasi kikubwa katika soka na, kwa maoni yangu, wamekuwa imara pia katika michuano ya kimataifa hivyo tunatarajia kucheza dhidi ya moja ya timu kubwa barani Afrika. Tunapaswa kuwa waangalifu na kujitolea kwa hali ya juu na kuonyesha umakini mkubwa ili tuweze kupata matokeo mazuri

"Kuhusu mchezaji Pacome, ni kweli kwamba ana majeraha. Sote tulishuhudia alipoyapata katika mchezo wetu dhidi ya JS Kabylie. Kwa sasa tunaendelea kufuatilia kwa karibu hali yake kiafya na baada ya mazoezi ya mwisho ya leo tutajiridhisha iwapo atakuwa tayari na sehemu ya kikosi kwa ajili ya mchezo wa kesho" Pedro Gonçalves.


TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804. 






Post a Comment

0 Comments