Na Ally Mandai.
Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimeleta maafa makubwa, huku mafuriko yakisababisha uharibifu wa makazi, miundombinu na mali za wananchi.
Hali imekuwa mbaya zaidi katika eneo la Turiani wilayani Mvomero,Mkoani Morogoro ambako kaya kadhaa zimelazimika kuhama makazi yao kutokana na maji kujaa ndani ya nyumba na mashamba kusombwa na maji.
Wananchi ambao ni waathirika wa mafuriko, akiwemo Diwani wa Kata ya Sungaji, Mji wa Turiani, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wamepaza sauti kuiomba Serikali iwatatue changamoto hiyo ya muda mrefu.
Wamesema kila msimu wa mvua hukumbwa na mafuriko yanayoathiri makazi yao, kuharibu mazao mashambani na kusababisha upungufu wa chakula.
Aidha, wameeleza kuwa mafuriko hayo pia huathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za kiuchumi, ikiwemo biashara ndogondogo na kilimo ambacho ndicho tegemeo lao kuu.
Kutokana na hali hiyo, wameitaka Serikali kuchukua hatua za kudumu kama kuboresha mifereji ya maji, kujenga kingo na kuandaa mpango maalum wa kuzuia au kupunguza athari za mafuriko katika eneo hilo.
TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804.



0 Comments