ISRAEL NA IRAN WAFUNGA ANGA ZAO

 Na Ally Mandai.

Israel imefunga anga yake kwa safari zote za ndege za kiraia kufuatia shambulio lililofanywa dhidi ya Iran mapema leo Jumamosi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, linalohusishwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), anga ya Iran nayo imefungwa.

Msemaji wa Shirika la Usafiri wa Anga la Iran, Majid Akhavan, amesema kuwa anga ya nchi nzima itabaki imefungwa hadi itakapotolewa taarifa nyingine rasmi.

Wakati huohuo, Wizara ya Afya ya Iran imetangaza kuwa hospitali zote zimewekwa katika hali ya tahadhari na maandalizi ya dharura, huku idadi ya majeruhi ikitarajiwa kutangazwa baada ya kukamilika kwa uhakiki rasmi.

TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804. 


 

 

Post a Comment

0 Comments