Na Ally Mandai.
Mahakama Kuu
Masijala ndogo ya Dar es imesema itafanyia marekebisho upya kizimba
kilichopo ndani ya Mahakama ili Shahidi wa Siri aweze kutoa ushahidi.
Hatua
hiyo imekuja baada ya pingamizi aliloliweka mshitakiwa Tundu Lissu
Novemba 12,2025 baada ya kukataa shashidi wa Nne wa siri wa upande wa
Serikali ambaye alikuwa anatoa ushahidi wake bila kuonekana na mtu
yeyote wakiwemo majaji wenyewe.
Akitoa uamzi huo,jaji
anayesimamia kesi hiyo Dustin Ndunguru amesema amri ya 3 inasema
kizimba maalum ya Shahidi ni sehemu ya kukaa au kusimama akiwa
anaonekana kwa majaji na kutokana na kizimba hicho kilivyo basi ni kweli
Shahidi hataonekana lakini Mahakama itafanyia marekebisho kizimba hicho
ili shahidi wa Siri aweze kuonekana kwa majaji kwa kuzingatia kifungu
cha 194 cha ulinzi wa mashahidi.
Amesema hoja ya Mshitakiwa ya
kwamba hatuweza kumhoji vilivyo Shahidi maswali dodoso (Cross
Examination) kwa kutokana na uwezo wa kutomuona, Jaji Ndunguru amesema
hoja hizo siyo za msingi kwani mshitakiwa atakuwa na uwezo wa kufanya
hivyo.
Ikumbukwe kuwa pingamizi hilo lilitolewa Novemba 12, 2025
na mshitakiwa Tundu Lissu kumpinga shahid wa Nne wa siri wa Serikali
aliyefahamika kwa jina la P11.
Kwa mantiki hiyo, Mahakama
imetupilia mbali mapingamizi yote yaliyotolewa na Mshitakiwa Tundu Lissu
na badala yake upande wa Mahakama itafanyia marekebisho kizimba hicho
ili shahidi aweze kuonekana.
Baada ya maamzi hayo,upande wa
Jamhuri uliomba kuahirishwa kwa shauri hilo,jambo ambalo lilipingwa na
mshitakiwa huku akiomba mashahidi wengine waje ili kesi iendelee.
Baada
ya maombi ya pande zote mbili,jopo la majaji limejadiliana na
kukubaliana kuwa Shauri litaendelea kesho Alhamisi saa tatu asubuhi.
0 Comments