Na Ally Mandai.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya
uteuzi wa wenyeviti wa bodi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka,
walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
(i) Mhe. Anne Samamba Makinda ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Wengine ni
(ii)
Bw. Jaffer Machano ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Shirika la Reli Tanzania (TRC). Bw. Jaffer anachukua nafasi ya Bw. Ally
Amani Karavina;
(ii) Dkt. Albina Andrew Chuwa ameteuliwa kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa
Kaboni (NCMC); na
(iv) Prof. Makenya Abraham Maboko ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
0 Comments