AMINA GOOD AKAGUA MIRADI YA UWT ILALA, DAR ES SALAAM

Mbunge wa Viti Maalum  Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkurugenzi wa AMO FOUNDATION Amina Good amefanya ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo ya Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) iliyopo Wilaya ya Ilala.

Dhumuni kuu la kuangalia miradi hiyo ya Jumuiya ni kuona namna gani kama Mbunge wa Mkoa wa Dar es salaam anaweza kusaidia ili isonge mbele.

Alitembelea Mradi wa Nyumba ya Katibu wa Wilaya Ilala iliyopo Kata  Mchikichini ambapo ameahidi kuhakikisha anachangia kukamilisha Ujenzi wa nyumba hiyo, mradi mwingine aliotembelea ni Viwanja vya Zingiziwa vilivyopoKata ya  Buguruni Mkoani humo.

Ziara hiyo ni moja ya mikakati yake ya kufatilia miradi mbalimbali ya UWT iliwemo kupambaia wanawakewa Mkoa wa Dar es Salaam katika kutatua changamoto zao sambamba na kuwawekea mazingira ya ujasiriamali na yanastawi.

 Hata hivyo ni hivi karibuni tu Good alifanya Semina kubwa ya kuwaandaa Wanawake wa Mkoa Dar es salaam kujitegemea kiuchumi ambapo  aliahidi kuandaa tukio la  kuwawezesha vifaamtaji ili wajikwamue kiuchumi kwa kupambanana changamoto za maisha.

Katika Ziara hiyo Amina Good ameambatana na Kamati ya Utekelezaji Wilaya ya Ilala chini ya Mwenyekiti wake Neema Kiusa pamojana  na Katibu wa Wilaya Rosemary Mwakisalu.





Post a Comment

0 Comments