AZAM FC WAUMALIZA MWENDO KIBABE SHIRIKISHO AFRIKA

 Na Ally Mandai.

Klabu ya Azam FC hii leo waondoshwa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) baada ya kukubali kichapo cha 2-0 mbele ya Wydad Casablanca katika Dimba la Mohamed V.

Azam Fc wameishia katika hatua ya makundi wakiwa na alama 9 ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Klabu hiyo kushiriki katika hatua ya Makundi na kumaliza wakiwa na alama 9.

FT: Wydad AC 2-0 Azam Fc
FT: Maniema 3-0 Nairobi United

MSIMAMO KUNDI B:
1. Wydad AC Alama 15
2. Maniema Alama 12
3. Azam FC Alama 9
4. Nairobi United Alama 0

NB: Azam Fc ndiyo timu kutoka Tanzania iliyokusanya alama Nyingi zaidi (9) katika michuano ya kimataifa CAFCC/CAFCL.




 

 

Post a Comment

0 Comments