Na Ally Mandai.
Simba SC wamehitimisha safari yao ya msimu huu wa CAF Champions League kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Stade Malien katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi. Ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa Simba katika kampeni hii, huku wakimaliza wakiwa na alama tano pekee.
Bao pekee la mchezo lilifungwa mapema kabisa dakika ya 4 kupitia kwa Oura A., bao lililodumu hadi dakika 90 kukamilika na kuwapa Wekundu wa Msimbazi tabasamu la mwisho katika mashindano hayo ya kimataifa.
Licha ya ushindi huo, msimu huu umebaki kuwa miongoni mwa misimu mibovu zaidi kwa Simba katika michuano hiyo, baada ya kukusanya alama 5 tu katika michezo sita waliyocheza hatua ya makundi.
Rekodi yao bora zaidi katika hatua ya makundi ilipatikana msimu wa 2020/21 walipomaliza na alama 13, wakionesha ushindani mkubwa dhidi ya vigogo barani Afrika wakiwemo Al Ahly SC.



0 Comments