Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dennis Londo (MB) amewaomba Viongozi wa Mkoa huo na Wananchi kuendelea kuwa Kitovu cha Utulivu na amani na Mkoa wa Kimkakati.
Naibu Waziri ametoa kauli hiyo leo Januari 7, 2026 alipofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huo kusaini kitabu cha wageni na kutumia fursa hiyo kutoa salamu za Wizara hiyo kwa mwaka huu mpya 2026 kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro.
Amesema, ingawa Serikali kazi yake kubwa ni kulinda Usalama wa Raia na mali zao kupitia Taasisi zake ambavyo kimsingi ni vyombo vya wananchi kama Jeshi la Polisi, Magereza, Jeshi la zima moto na Uhamiaji bado kazi hiyo itakuwa na ufanisi zaidi kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha na wananchi wake.
“Na sisi kazi yetu ni kuimarisha misingi ya mahusiano kati yetu Wizara, vyombo vyetu na wananchi wetu”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima Pamoja kutumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara hiyo kwa maboresho makubwa yaliyofanyika kwa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Polisi, Magereza, Jeshi la Zima Moto na Uhamiaji, bado amekuwa na baadhi ya maombi mahususi.
Moja ya jambo ambalo ameiomba Wizara hiyo ni kutumia jicho la tatu kuangalia uwezekano wa kuendelea kuboresha na kujenga miundombinu ya Magereza katika Wilaya za Malinyi, Kilosa na Gairo ambapo bado kuna changamoto katika Sekta hiyo.

0 Comments