NAIBU WAZIRI WA MAJI MHE. KUNDO MATHEW AWAHIMIZA BUWSSA USHIRIKIANO NA MATUMIZI YA DIRA JANJA

 Naibu Waziri wa Maji Mhe.  Mhandisi Kundo Mathew (Mb) amezungumza na wstumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) na kuwasisitiza ushirikiano katika utekekezaji wa majukumu yao. 

Amewasisitiza kuwa wizara inazo sifa njema za watumishi wa mamlaka hiyo, hivyo waendelee kujituma na kulinda heshima hiyo waliyokwisha ijenga. 

Aidha amesisitiza matumizi ya teknolojia ikiwemo matumizi ya dira za malipo kabla.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kuanza kutumia Dira janja hivyo wajikite katika eneo hilo.

Post a Comment

0 Comments