Na Ally Mandai
Marekani ilishambulia Venezuela usiku kucha na kumkamata Rais wake aliyehudumu kwa muda mrefu, Nicolas Maduro, Rais Donald Trump alisema mapema leo Jumamosi baada ya miezi kadhaa ya kumshinikiza kufuatia tuhuma za biashara ya dawa za kulevya na kukosa uhalali wa kushika madaraka.
Washington haijafanya
uingiliaji wa moja kwa moja kama huo katika Amerika ya Kusini tangu
uvamizi wa Panama mwaka 1989 uliolenga kumuondoa madarakani kiongozi wa
kijeshi Manuel Noriega, kwa tuhuma zinazofanana.
“Marekani
imefanikiwa kutekeleza shambulio kubwa dhidi ya Venezuela na kiongozi
wake, Rais Nicolas Maduro, ambaye yeye pamoja na mke wake wamekamatwa na
kusafirishwa nje ya nchi,” Trump alisema katika chapisho lake kwenye
Truth Social.
Marekani
ilikuwa imemtuhumu Maduro kuendesha “dola la mihadarati (narco-state)”
na kupanga matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana, ambao upinzani ulisema
uliushinda kwa kishindo.
Kiongozi
huyo wa Venezuela, aliyerithi madaraka kutoka kwa Hugo Chavez mwaka
2013, amesema Washington inataka kudhibiti hifadhi ya mafuta ya
Venezuela, ambayo ni kubwa zaidi duniani.



0 Comments