Na Ally Mandai,Facebook.
Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Awesu Awesu, ametambulishwa rasmi na Kenya Police FC kama mchezaji wao mpya.
Awesu
amejiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Kenya akitokea Simba SC,
katika uhamisho wa mkopo wa miezi sita, unaolenga kumpa nafasi ya kupata
dakika nyingi za kucheza pamoja na kuendelea kukuza ki-wango chake cha
mchezo.
Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa pande zote mbili,
ambapo Simba SC inaamini kuwa Awesu atanufaika kwa kupata uzoefu zaidi
wa ushindani wa ligi, huku Kenya Police FC ikipata mchezaji mwenye ubora
wa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.
Awesu anatarajiwa
kuanza kuisaidia Kenya Police FC katika malengo yao ya kutetea ubingwa,
huku mashabiki wa klabu hiyo wakimsubiri kuona mchango wake ndani ya
uwanja.
0 Comments