YANGA YANASA STRAIKA MUANGOLA




NA MOHSIN JUMA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga,wameanza mazungumzo na mshambuliaji Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depú’ anayechezea klabu ya Vojvodina ya Ligi Kuu ya Serbia kutoka Gil Vicente ya Ureno ili kupata saini yake kuelekea dirisha dogo la usajili.
Nyota huyo ni mchezaji ambaye kwa muda mrefu amekuwa kwenye darubini ya wataalamu wa scouting wa Yanga, wakimtazama kama chaguo la kuongeza kasi, ushindani na ubunifu kwenye eneo la ushambuliaji ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Depu ambaye ni mfungaji bora wa michuano ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA)mwaka huu tayari amefikia patamu mazungumzo yake na viongozi wa Yanga akionesha utayari wa kutua mitaa ya Twiga na Jangwani kuongeza nguvu katika kikosi cha timu hiyo.Nyota huyo mwenye miaka 25 alimaliza michuano hiyo akipachika wavuni mabao nane na kuibuka mfungaji bora sambamba na kuiwezesha timu ya Taifa ya Angola kutwaa taji hilo.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga,zinaeleza,Depu ambaye ni mkali wa kufunga mipira ya kutenga,vichwa na pasi ndefu amewaambia mabosi wa Yanga yuko tayari kutua Jangwani na kinachoendelea kwa sasa ni majadiliano ya baadhi ya vipengele vya mkataba wake baada ya kuikubali ofa aliyopewa.

Kama Depu atatua Yanga, basi tatizo la mipira ya juu na ya kutengwa linaweza kugeuka kuwa silaha ya kuangamiza maadui.Mmoja ya wachambuzi nguli wa soka nchini Ramadhani Mbwaduke ameuangalia usajili wa nyota huyo na kusema kwa siku za hivi karibuni Yanga imekua inazalisha mipira mingi ya juu langoni mwa wapinzani wake lakini imekua ikikosa utekezaji wa usahihi. 
Mbwaduke anasema katika mechi mbili za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika(CAF CL)hatua ya makundi,Yanga walipiga krosi 28 lakini sita tu zikamfikia mchezaji ndani ya boksi licha ya kuwa na watengenezaji wengi kama Kibwana Shomari,Israel Patrick Mwenda,Shedrack Boka na Mohamed Hussein Tshabalala.

Kwenye pasi ndefu nako ni shida: 85 zilipigwa, 36 tu zikafika, na kati ya hizo, pasi moja tu ndiyo ilizalisha shambulio la moja kwa moja.Ukimuangalia DEPU akiwa na Angola; alikuwa Mfungaji Bora wa COSAFA, ndani ya mechi tano akifunga mabao nane. Ukija Ligi Kuu ya Poland akiwa na RSK Domiak, mechi tisa amepiga mashuti tisa, matatu ON TARGET na moja likiwa goli, huku mabao yake mengi yakitokana na mipira ya juu na pasi ndefu.

Post a Comment

0 Comments