Tetesi zinaeleza kuwa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Yanga SC wameanza kumtolea macho winga wa Simba SC,Morice Abraham kuona kama wanaweza kumpata kupitia dirisha dogo la usajili.
Yanga wako katika mchakato wa kuboresha kikosi Chao kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutetea taji lao Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga SC kwenye ligi ya mabingwa Afrika inataraji kucheza dhidi ya Al Ahly mwezi Januari ikiwa ni michezo miwili mfululizo wakihitaji kufanya vyema kwenye michezo yote hiyo.

0 Comments