SERIKALI ITAHAKIKISHA MIRADI YOTE YA UMWAGILIAJI INAKAMILIKA KWA WAKATI- MHE. DANIEL CHONGOLO


Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo, ametembelea mradi wa Umwagiliaji uliopo wilayani Masasi mkoani Mtwara ikiwa moja ya muendelezo wa ziara kwa Taasisi za Wizara ya kilimo ambapo amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itakikisha miradi yote ya Umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima.

Serikali itahakikisha miradi yote ya Umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima hali itakayoimarisha uchumi na kuleta uhakika wa chakula.

Mhe. Chongolo amesema hayo wakati wa ziara yake katika mradi huo unaotekelezwa eneo la Ndanda, mkoani Mtwara. 

Mradi huo unahusisha ujenzi wa bwawa la Umwagiliaji na uchimbaji wa mifereji mirefu, na ukikamilika unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wakulima 700 kutoka vijiji saba.

“Serikali itahakikisha miradi yote ya Umwagiliaji inakamilika na kuleta tija kwa wakulima hali itakayoimarisha uchumi na kuleta uhakika wa chakula, amesisitiza.

Amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa bwawa hilo ambalo litachochea matumaini mapya kwa wakulima wa Mtwara kwa kuwawezesha kulima mazao mbalimbali ikiwemo mboga mboga, mpunga, mahindi na mazao mengineyo.

Ameongeza kuwa ingawa Mtwara inasifika kwa kilimo cha korosho, serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imeanzisha miradi ya Umwagiliaji katika mikoa ya Lindi na Mtwara ili kuhamasisha uzalishaji wa mazao mengine ndani ya mikoa hiyo bila kutegemea mazao kutoka maeneo mengine.

Aidha, Mhe. Chongolo ameisihi Tume kusimamia kwa umakini miradi hiyo ili kuhakikisha thamani ya fedha iliyowekezwa inaonekana na wakulima wanapata uzalishaji unaoendana na viwango vinavyotakiwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainabu Telacky amewataka wananchi kushirikiana na Tume katika kulinda miundombinu na rasilimali zilizowekezwa na serikali kwa kuwa wao ndio wanufaika wakuu wa mradi huo.


 

Post a Comment

0 Comments