DKT. SHEIN ATAKA UMMA KUELIMISHWA ZAIDI KUHUSU FAIDA ZA MUUNGANO

 Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Saba Dk. Ali Mohamed Shein ameitaka Ofisi ya Makamu wa Rais kufanya jitihada ya kimaksudi ya kuendelea kuelimisha wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu faida ya umoja uliokuwa kwenye Muungano kwani itasaidia kuudumisha Muungano wetu.

Mhe. Dkt. Shein ameyasema hayo wakati akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni mara alipomtembelea nyumbani kwake Zanzibar, Disemba 10,2025. Mhe. Mhandisi Masauni aliambatana na viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.








Post a Comment

0 Comments