WAZIRI GWAJIMA AFANYA KIKAO KAZI NA DC UBUNGO
Leo Desemba 22, 2025 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amefanya kikao cha majumuisho mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam.
Kikao hicho kimejikita katika kupitia na kujadili hatua za utatuzi wa changamoto zilizoibuliwa na vikundi vya wanawake wakati wa ziara hiyo, ikiwemo changamoto za upatikanaji wa mikopo ya Serikali, uelewa mdogo wa taratibu za mikopo, pamoja na vikwazo vya kiutawala vinavyokwamisha utekelezaji wa miradi ya uwezeshaji wanawake kiuchumi.
Aidha, Dkt. Gwajima ametoa elimu na maelekezo mbalimbali kwa vikundi hivyo, akisisitiza umuhimu wa kuwa na maandiko sahihi ya miradi, usimamizi bora wa mikopo, nidhamu ya marejesho pamoja na kushirikiana kwa karibu na Maafisa Maendeleo ya Jamii ili kuhakikisha wanapata taarifa sahihi na huduma kwa wakati.

0 Comments