SAFARI YA MWANAMUZIKI DR REMMY ONGARA (1)



sehemu ya kwanza


NA:DAUDI KISUGURU.


DR REMMY alizaliwa tarehe10/2/1947.Baba yake Remmy alifahamika zaidi kwa upigaji wa ngoma kwenye sherehe mbalimbali alikuwa anaitwa ETIENNES KALIMANGONGA ambaye alikuwa anatoka katika kabila la MKUSU kutoka watu wa kindu manyema(ambao ni sehemu ya kabila la wamanyema wa kigoma) katika jimbo la kivu, Zaire wakati huo DRC sasa.

Baba yake Remmy alipigana vita kuu ya pili ya dunia mwaka (1939-1945), baada ya vita MZEE KALIMANGONGA akapewa kiinua mgongo na akahamia kilometa 25 kutoka KISANGANI mjini.


Mama yake na dr Remmy alikuwa anaitwa AZIZA MOZA MAYOKEI kutoka kabila la walengola alikuwa binti wa chifu kimbebe, alifariki mwaka 1964.Dr Remmy akiwa na umri wa miaka 17 kwa mama na baba huyu walizaliwa watoto wawili yaani Ramadhani na FARANGA MWANGAZA dada yake Remmy aliyezaliwa 1949.


Baada ya kufariki mzee kalimangonga mpiga ngoma na   mwanajeshi mstaafu Remmy akiwa kijana wa miaka 9 mama yake aliolewa na bwana mwingine aitwae AMANI huyu pia alikuwa wa kabila la mlengola.Wakazaliwa ndugu watatu wa Remy ambao ni AZIZA,MARIA na JOHN AMAN.Remmy alisoma mpaka darasa la tano 

katika shule ya ECOLE LAIC(shule ya laic) ilikuwa katika kanda ya LUBUNGA huko huko kisangani ilikuwa shule ya mseto wa wazungu na waafrika vilevile mseto wa wavulana na wasichana.


Elimu ilifundishwa kwa kifaransa na kiswahili.Mwaka 1964 baada ya kusumbuliwa sana na pumu mama yake Remmy alifariki Remmy akiwa na umri wa miaka 17.Hapo ikabidi Remmy aache shule na kwa kuwa hakuwa na ndugu anaowategemea na Kisangani kulikuwa na machafuko ya kidini na kisiasa mambo haya yalimwathiri sana Remmy kifikra na kifalsafa.


BENDI YA KWANZA YA REMMY.

Basi alikuwapo tajiri mmoja mwenye bar mjini kisangani  kwa jina LUANGE 

bar yake nayo iliitwa luange. Alimnunulia Remmy vyombo vya muziki,vyombo ambavyo inasemekana vilikuwa vinatumiwa na DR NICKO KASANDA na kuanzisha bendi yake ya kwanza iliyoitwa SUCCESS BANTU ikiwa na wanamuziki sita.Yeye Remmy alikuwa ndiye kiongozi,muimbaji na mpiga solo.

    SUCCESS BANTU chini ya uongozi wa Remmy yenye vyombo vya tajiri luange mwenye luange bar ilivuma mjini Kisangani na wakati huu Remmy akatunga nyimbo zake za mwanzo mwanzo,uliopendwa zaidi ulikuwa  ukiitwa "HEA" katika lugha ya kilingala

uliokuwa na maana ya "nasikitikia maisha yangu".Hapa Dr Remmy alikuwa anaelezea machungu ya maisha yake hasa baada ya wazazi wake kufariki na hasa mama yake mzazi na yeye kushindwa kuendelea na masomo.


Elimu kama huduma nyingine za Zaire iliyojitawala punde, matibabu, usafiri na kadhalika ilikuwa jambo la kulipiwa kama hukuwa na fedha huwezi kuzipata.Hivyo watu wa matabaka ya chini wakulima na wafanyakazi walitota chini ya ukosefu wa elimu na afya.

   

Hata hivyo Remmy hakudumu muda mrefu na bendi ya success bantu

mwaka 1968 alihamia bendi ya SUCCESS MUACHANA baada ya bendi ya success bantu kumpata mpiga solo mahiri zaidi ya Remmy.


Vyombo vya success muachana vilikuwa mali ya tajiri LUKOLO,tajiri mwingine wa mjini KINDU katika jimbo la mashariki zaidi ya KISANGANI yaani

KIVU.Ndani ya bendi hii walikuwapo wanamuziki wenye ujuzi zaidi ya bendi ya mwanzo ya Remmy.

Alikuwapo NKASHAMA NKOI kwa mfano ambae baadae alikuja kuwa mashuhuri siyo Zaire tu bali hadi Kenya na Tanzania huyu alikuwa mwimbaji, alikuwapo jamaa aliyekuwa anapiga solo gitaa kwa jina anaitwa FRANKIE,

hapa dr Remmy alikuwa anaitikia sauti ya pili na kupiga drums.Ila Remmy aliendelea na utunzi katika bendi hii alitunga wimbo mmoja uliokuja kuwa mashuhuri unaitwa

"Nalingakate koswana nabaninga"

wenye maana sipendi kugombana na watu.Mwaka 1970 baada ya miaka sita ya uzoefu wa muziki akajiunga na bendi ya GRAND MICKY ambayo alikaa nayo kwa muda miaka minane hadi alipohamia TANZANIA mwaka 1978.


Post a Comment

0 Comments