Siku moja baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani kati ya Kinshasa na Kigali nchini Marekani, mapigano mengi yameendelea kurindima mashariki mwa DRC. Milipuko kadhaa ilisikika katika maeneo kati ya Bukavu na Uvira, katika jimbo la Kivu Kusini.
Kulingana na ripoti kadhaa za Umoja wa Mataifa, hasa katika mkoa wa Kivu Kusini, mvutano wa usalama naendelea kuongezeka huko Kaziba na uwanda wa Mto Ruzizi kati ya AFC/M23 inayoungwa mkono na Rwanda na jeshi la Kongo, linaloungwa mkono na wanamgambo wa Wazalendo na jeshi la Burundi.
Mapigano mengine pia yameripotiwa mbali kidogo magharibi, kwenye vilima vinavyoelekea kijiji cha Kaziba, katika eneo la Walungu, ambapo wakazi wengi waliokuwa wamejificha katika nyumba zao tangu katikati ya wiki wamehama, anasema mwandishi wa habari kutoka kituo cha redio cha eneo hilo aliyekimbia.

0 Comments