Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ashiriki Doha Forum




Rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete, ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education (GPE), ameshiriki jukwaa la Doha Forum 2025 ambapo amesisitiza umuhimu wa elimu bora na stadi za kidijitali katika kuwawezesha vijana wa Afrika kujibu mabadiliko ya kiuchumi yanayokumba bara.


Katika jopo lililoongozwa na Kikwete, washiriki wengine walikuwa Rais wa Ghana John Dramani Mahama, Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo na wataalamu wengine wa kimataifa. 

Kikwete alisema elimu yenye ubora ndiyo msingi wa ustahimilivu wa kiuchumi na maendeleo endelevu barani Afrika.

Post a Comment

0 Comments