Waziri wa zamani wa viwanda na biashara Geoffrey Mwambe ameachiwa kwa dhamana na jeshi la polisi jana 14 Disemba 2025.
Hayo yamebainishwa na wakili Hekima Mwasipu leo 15 Desemba 2025 na kusema mteja wake anakabiliwa na tuhuma mbili za makossa ya jinai ikiwemo kutuhumiwa kumtishia kumuua kamanda mkuu wa polisi ambaye hata hivyo hajatajwa jina lake na tuhuma za kiuchochezi za kimtandao.
Wakili Mwasipu amesema maombi waliofungua dhidi ya jeshi la polisi ya kumpatia Mwambe dhamana ambayo yalitarajiwa kufanyika leo 15 Disemba katika Mahakama ya hakimu mkazi kisutu hayana nguvu tena kwa sababu mteja wake yupo huru.
Kwa upande mwingine Wakili Mwasipu amesema Mwambe ataendelea kuripoti katika ofisi ya ZCO katika kipindi hiki ambacho upelelezi unaendelea na kama atabainika kuwa na kosa,basi atafikishwa Mahakamani.webp)
.webp)
0 Comments