MWISHO WA KULIPA ADA YANGA DESEMBA 31

 Klabu ya Yanga kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Wanachama Ibrahim Samwel amesema Disemba 31, 2025 ndio utakuwa mwisho wa kulipa ada ya uanachama kwa wanachama wote wa Yanga SC kwa wale wa nje ya Tanzania na ndani ya Tanzania.


"Yanga SC yetu itafanikiwa zaidi kama tutajiimarisha zaidi kiuchumi, wanachama wenye asilimia 51% ndio tuna nafasi kubwa ya kuhakikisha tunaichangia timu yetu."- Ibrahim Samwel (@i_sammjr ) Mkurugenzi wa Wanachama Yanga SC.


"Yanga SC sisi tumeweka utaratibu na sheria tunapofungua msimu mpya wa kulipia ada zoezi hilo litaenda kwa miezi pekee, hivyo tunawaasa viongozi wa matawi wawahimize watu wao walipe ada zao mapema kuepuka kuwa wadaiwa sugu, miezi sita ambayo tumeweka tangu tumefungua msimu mpya wa kulipia ada unaisha Disemba 31, 2025."- Ibrahim Samwel (@i_sammjr ) Mkurugenzi wa Wanachama Yanga SC.

Post a Comment

0 Comments