Na Ally Mandai
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mheshimiwa Edward Mpogolo amefungua rasmi mafunzo ya siku tatu ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam huku amewataka waheshimiwa madiwani hao kwenda kua kiunganishi baina yao na watendaji wa mtaa na wenyeviti wa serikali ya mtaa pamoja na wananchi.
Akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya peacock Mhe. Mpogolo amesema mafunzo hayo yawe na tija kwa kuwatumikia wananchi katika maeneo yao.
Ukijua shida za watu wako huwezi kuona mzigo kuhudumia watu hao, nendeni katatueni kero za wananchi katika maeneo yenu
Jumla ya mada kumi zilijadiliwa katika mafunzo hayo ya siku tatu yalioendeshwa na wakufunzi kutoka chuo cha Uongozi cha Hombolo yalikua na lengo la kuwajengea uwezo Madiwani hao juu ya uendeshaji wa mamlaka za serekali za mitaa.

.jpeg)



0 Comments