NA MWANDISHI WETU
STRAIKA wa Klabu ya Simba SC, Jonathan Sowah, amefungiwa michezo mitano na kutozwa faini ya Shilingi 1,000,000 kwa kosa la kufanya kitendo kisicho cha kiuanamichezo, baada ya kumpiga kiwiko mchezaji Himid Mao wa Klabu ya Azam FC.
Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 41:21 ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayohusu udhibiti wa wachezaji.
Vilevile, mchezaji mwingine wa Klabu ya Simba SC, Allasane Kante, inayotokea mkoani Dar es Salaam, naye amefungiwa michezo mitano na kutozwa faini ya Shilingi 1,000,000 kwa kosa la kufanya kitendo kisicho cha kiuanamichezo, baada ya kumpiga teke kwa makusudi mchezaji Feisal Salum wa Azam FC.
Maamuzi hayo yanatokana na matukio yaliyotokea wakati wa michezo ya Ligi Kuu baina ya timu hizo yakilenga kudhibiti nidhamu na kuimarisha maadili ya michezo.
@@@@

0 Comments