JK AWASILI KANISANI KUAGA MWILI WA JENISTER MHAGAMA

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, pamoja na viongozi mbalimbali, wamewasili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kiwanja cha Ndege, jijini Dodoma, kushiriki ibada na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Jenista Mhagama.

Marehemu alikuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho tangu mwaka 2005 na amefariki dunia siku ya Alhamisi, tarehe 11 Desemba, 2025, jijini Dodoma katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa tarehe 14 Desemba, 2025 kuelekea Songea, ambako mazishi yatafanyika siku ya Jumanne, tarehe 16 Desemba, 2025, katika kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma.

 

Post a Comment

0 Comments