IBENGE NI BINGWA WA KUBADILI GIA ANGANI

Niliwahi andika siku moja sifa kubwa zaidi ya kocha hasa kwa mpira wa kisasa uliojaa mbinu ni _READING THE GAME_. Kazi ya kuipa timu Physique , Tactics na Technique ni wazi Kila kocha anaweza kujua kwani ndio msingi wa ualimu wa mpira wa miguu . Tofauti kati ya kocha na kocha ni hiyo👆kuweza kusoma mchezo tena mchezo unaoendelea mbele ya macho yako bila kujali pressure kubwa Kwa wakati huo. Sifa hii ni muhimu sana Kwa kocha kuwa nayo kwani ndiyo inaleta thamani halisi ya kocha. Na ndiyo maana ulaya wao kocha wanamuita MENEJA sababu ana meneji idara zote za coaching (fiziki,tekiniki,saikoloji, nutrition, goalkeeping) vyote hivi vifanyike Kwa kiwango na ubora anaoutaka yeye ili yeye amalizie kuweka tactics ktk hiyo timu.Hivyo utagundua modern coach ni yule anayeweza kuipiganisha mechi akitumia wachezaji wake ambao wameandaliwa kwa ubora ambao anauhitaji kiwanjani.Hii sifa ni dhahiri shahiri Kwa makocha wa timu za Taifa ambao hawana muda mrefu wa kukaa na wachezaji wao badala yake anapowaita kwenye timu tayari anajua atawatumiaje. *_IBENGE_* ana u *_DELEBOSQUE_* flani hivi ( kocha wa zamani wa Madrid na Spain) muda mwingi yuko kimya kwenye benchi kakaa au kasimama lakini muhimu ni kuangalia Kila sekunde inaendaje kwenye uwanja wa mechi. Game plan yangu inafanya kazi? Kwanini haifanyi kazi? Tatizo ni Mchezaji mmoja au idara nzima( defence mid attack)?au tatizo ni wapinzani? Kama tatizo ni wapinzani Je? ni Mchezaji wao mmoja ( fundi) au ni idara yao iko bora kuliko yangu? au tatizo ni Game plan ya mpinzani iko bora kuliko yangu ? Je? kwahiyo Kuna haja ya kufanya mabadiliko sasa au nisubiri HT ( unapima madhara) . Kwa uchache maswali ambayo makocha huwa tunajiuliza wakati mechi inaendelea Kwa ulaya ni rahisi kwani Kuna watu humsaidia kocha kujibu baadhi ya maswali haya lakini bado kocha ni overall. *_IBENGE_* alifanikiwa kujiuliza na kujijibu maswali haya lakini kubwa zaidi _alimsoma_ pia *_MATOLA_* akamuona kamaliza ikawa kazi rahisi kwake kubadili mchezo Kwa kufanya mabadiliko muhimu na sahihi kuingia Kwa Akaminko akatulize dimba ili Himid afanye Kwa ufanisi kazi ya kuwalinda walinzi na Saadun akiwa ful energy akimbie _wide left_ dhidi ya Kapombe(Kalabou+Nangu) ambaye keshatumika dakika nyingi kiwanjani . Ulishawahi kukutana na *_KOCHA MTANGAZAJI_*???(rukaaa....kimbiaaaa....twende twende twendeee.....tukabeee) Ukimuuliza why atakujibu wachezaji wetu lazima wa pushiwe kumbe hajui anawalemaza na kuwajengea hofu ya kuogopa kukosea.

Post a Comment

0 Comments