Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo mapema leo tarehe 11 Desemba 2025.
Katika taarifa ya Mkoa, Kanali Sawala amemueleza Waziri Chongolo hali ya usalama wa chakula kuwa nzuri kwani mkoa una ziada ya chakula.
“Serikali ya Mkoa tunawasisitiza wananchi kulima mazao mchanganyiko ikiwemo na chakula, ili pesa iliyopatikana kwa kuuza korosho itumike kwa shughuli za maendeleo badala ya kutumia kununua vyakula.” Alieleza Kanali Sawala
Hii ni ziara ya kwanza kwa Waziri Chongolo tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.






0 Comments