Bajaber Aanza Kutupia,Simba ikifunga Mbeya City

Na Mwandishi Wetu

Kiungo mpya wa Simba SC, Mohamed Bajaber, ameanza kwa kishindo katika mechi yake ya kwanza akiifungia bao zuri kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Mbeya City, mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa leo.

 

Bajaber aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Elie Mpanzu, na dakika chache tu baada ya kuingia uwanjani, alionyesha thamani yake. 


Pasi ya kwanza kabisa aliyopokea kutoka kwa straika Jesse Mukwala aliigeuza kuwa bao la tatu kwa Simba, na kuhitimisha karamu ya mabao ya Wekundu wa Msimbazi.

Mashabiki wa Simba walionekana kufurahishwa na kiwango cha Bajaber, wakisema kijana huyo anaonyesha dalili ya kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi hicho. 

Kocha wa Simba Selrman Matola amepongeza utulivu na uamuzi wa haraka wa Bajaber uwanjani, huku akisisitiza kuwa bado ana mengi ya kuonyesha kadri anavyoendelea kuzoea mazingira ya timu.



 

Post a Comment

0 Comments