UONGOZI wa Yanga umeanza upya mchakato wa kutafuta kocha wa timu hiyo baada ya kufunga uwezekano wa kumchukua kocha Romuald Rakotondrabe ‘Roro’ aliyekuwa anakaribia kutua katika timu hiyo, huku Nasreddine Nabi akitia mkono.
Uamuzi huo unakuja baada ya Yanga kuachana na aliyekuwa kocha wao Romain Folz, baada ya timu hiyo kupoteza mechi ya kwanza msimu huu ikifungwa bao 1-0 ugenini dhidi ya Silver Strikers ya Malawi.
“Sio taarifa nzuri kwa Yanga kupoteza kocha wakati huu, kuna presha inaongezeka kwa uongozi na hata timu, lakini naamini wanaweza kurudi kwenye utulivu. Siku zote naamini katika hatua zao,”
“Nilikuwa hapo Tanzania, niliwaona (Yanga) sina tatizo na ubora wa wachezaji wao hata kocha, lakini nadhani wanahitaji kocha mwenye uzoefu mkubwa anayeweza kuisimamia klabu yenye presha ya matokeo kama Yanga.
“Nilivyowaona ni kama wachezaji walikuwa hawaogopi kucheza nje ya maelekezo, wanahitaji kocha ambaye akiwa nje amesimama wachezaji wake watakuwa wanakumbuka kile wanachotakiwa kufanya.”
