Kulingana na wanafamilia wa karibu na maafisa wa Ikulu wanaohusika moja kwa moja na mipango ya mazishi ya Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Amolo Odinga, aliacha wosia kwamba azikwe ndani ya saa 72.
Tayari maandalizi ya mazishi yanapangwa kufuatana na wosia huo, ambapo kama utafuatwa basi atazikwa Jumamosi.
Raila Odinga, ambaye alikuwa akitibiwa nchini India, alifariki leo baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.
Alikimbizwa hospitalini ambako alitangazwa kufariki mwendo wa saa 9:52 asubuhi (saa za India), kulingana na Msemaji wa hospitali hiyo.
