MPINA AGONGA MWAMBA URAIS 2025 NDIO BASI TENA

 Kesi ya Luhaga Mpina na ACT-Wazalendo kuhusu pingamizi la kuenguliwa kwenye nafasi ya kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 imetupiliwa mbali ambapo Mahakama imeeleza kuwa kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya nchi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haipaswi kuingiliwa na chombo chochote kwa jambo ambalo ilifanya kwa nia njema.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Oktoba 15, 2025 mbele ya  Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma na kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo Jaji Fredrick Manyanda. Majaji wengine waliosikiliza kesi hiyo ni Sylvester Kainda na Abdallah Gonzi.

Kwa uamuzi huo, Mpina hataweza kushiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu, ambao kwa sasa vyama vya siasa vinavyoshiriki vinaendelea na kampeni.



Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form