Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ameahidi kuwa endapo chama hicho kitapewa ridhaa ya kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, changamoto ya maji katika Wilaya ya Ilala na Jimbo la Segerea itabaki kuwa historia.
Katika mkutano wa kampeni uliofanyika Jimbo la Segerea jana, Dk. Nchimbi alieleza kuwa Serikali ya CCM itawekeza kwenye mradi mkubwa wa kuzalisha na kusambaza maji.
Hiyo ni pamoja na kupanua mtandao wa mabomba na kubadilisha mabomba yote yaliyoharibika chini ya ardhi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.
Aidha, ametangaza mpango wa kujengwa tanki kubwa la maji litakalohudumia Jimbo la Segerea.
Kwa sasa tanki hilo lina ujazo wa mita za mraba 273 pekee.
Tanki hilo litapanuliwa mara nne hadi kufikia ujazo wa mita za mraba 845 milioni ili kukidhi mahitaji ya wakazi.
Dk. Nchimbi pia alitumia fursa hiyo kuwanadi wagombea ubunge wa mkoa huo, akiwemo Mgombea wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli, pamoja na wagombea udiwani wa kata.
