Waziri wa
Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, amewataka wakurugenzi na
menejimenti ya wizara hiyo kuongeza ubunifu na kuibua fursa
zitakazosaidia wananchi kutatua changamoto zao.
 |
Waziri wa katiba na sheria,Ndumbaro akiongoza kikao kazi katika chuo cha uongozicha Mwl.Nyerere kibaha,Pwani. |
Waziri Ndumbaro
alisisitiza kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ni wizara ya utawala na
usimamizi wa haki, akihimiza umuhimu wa kuhakikisha majukumu
yanatekelezwa kwa wakati na kwa weledi.
Ndumbaro Alisema hayo
siku ya jana Julai 18, 2025 katika Kikao Kazi kinachofanyika katika
Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere, Kibaha, Pwani, ambacho kinalenga
kutathmini utendaji wa wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kuweka
mikakati mipya ya kuongeza ufanisi kwa mwaka 2025/2026.
Akifafanua
zaidi, Waziri Ndumbaro alibainisha kuwa kutokana na uwepo wa Dira ya
Taifa 2050, wizara haina budi kuanza kuweka mikakati ya kutekeleza
mipango yake kwa kuihusianisha na maono na misingi mikuu iliyobainishwa
katika dira hiyo. Alitaja misingi hiyo kuwa ni pamoja na:Kusimamia
misingi ya Utawala Bora,Amani, Usalama na Utulivu kwa Kuheshimu Katiba,
Demokrasia, Sheria na Haki za Msingi
Awali, Katibu Mkuu wa
wizara Ndg. Eliakim Maswi alisema kuwa kikao kazi hiki kitajumuisha
uwasilishwaji wa mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukumbushana
majukumu ya kiongozi bora,utendaji kazi na usimamizi wa rasilimali za
Serikali.
Kikao kazi hiki muhimu kinajumuisha timu ya viongozi
wa wizara, wakurugenzi wa idara, na vitengo na kinatarajiwa kuweka
msingi imara wa utekelezaji bora wa majukumu ya wizara katika kipindi
kijacho.