Waziri wa
Madini, Mh. Anthony Mavunde (Mb) amebainisha kuwa Mh. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelekeza kutolewa kwa
leseni ya uchimbaji madini ya nikeli kwa Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) na kwa Wachimbaji wadogo waliokuwepo katika eneo la vilima vya
Ntaka- Nachingwea, Mkoani Lindi.

Waziri Mavunde ameyasema hayo
leo tarehe 08 Julai, 2025 katika mkutano wa hadhara wa wananchi na
wachimbaji katika Kijiji cha Nditi punde tu baada ya kufanya ziara ya
kutembelea maeneo na migodi ya wachimbaji wadogo chini ya Umoja wa
Vikundi vya Wachimbaji Madini (UVIWAMA).
"Rais Dkt. Samia S.
Hassan amesikia kilio chenu cha muda mrefu cha kutaka kupewa maeneo ya
uchimbaji katika Leseni inayomilikiwa na Serikali. Na ndiyo maana
nimefika hapa kuja kuwaletea habari njema wachimbaji wadogo kwamba,
hatutawaondoa katika eneo mnalochimba na tunakwenda kuwarasimisha.
Pamoja
na kupewa eneo la uchimbaji, naomba niwasihi wachimbaji wadogo kufuata
taratibu kwa mujibu wa Sheria ya Madini Sura ya 123 ambayo inaelekeza
mwenye haki madini kuhakikisha anapata ridhaa ya mwenye haki ardhi kabla
hajaanza uchimbaji, ili kuepusha migogoro katika shughuli zao za
uchimbaji.
Rais Dkt. Samia ameelekeza eneo la leseni hiyo lenye
ukubwa wa Kilometa za Mraba 45 ipewe Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) kwa ajili ya kuanza uchimbaji mkubwa wa nikeli ndani ya miezi
18 ijayo kama Sheria ya Madini inavyoelekeza.
Kwa kuwa kwenye
Leseni hii serikali ililipa zaidi ya shilingi bilioni 243 kama fidia, ni
lazima sasa STAMICO na wachimbaji wadogo wafanye uchimbaji wenye tija
ili kurejesha fedha hizo katika mfuko mkuu wa Serikali”Alisema Mavunde
Awali,
akitoa salam kwa niaba ya wachimbaji wadogo, Mwenyekiti wa Chama cha
Wachimbaji Wadogo Mkoa wa Lindi (LIREMA), Bw. Mayunga Musa Buyaga
amesema wachimbaji wadogo wanamshukuru sana Rais Dkt. Samia S. Hassan
kwa upendo mkubwa na kuwajali na kuahidi kuendelea kushirikiana na
Serikali kwa kufanya uchimbaji wenye tija.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Mh. Zainab Telack* amempongeza Mh. Rais Dkt Samia kwa kurudisha
matumaini na nyuso za furaha kwa wachimbaji wadogo na kuahidi kuwa
Serikali ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati