WAZIRI MAJALIWA:TUILINDE AMANI KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani huku akiwahakikishia kuwa serikali itatekeleza wajibu wake ipasavyo.

"Nitoe rai kwa kila mmoja wetu kuhakikisha kila mmoja analinda na kuitunza tunu ya amani na utulivu wa nchi kabla wakati na baada ya uchaguzi.”

Akizungumza Bungeni leo juni 26 Majaliwa amesema serikali imejiandaa vyema na itahakikisha inasimamia uchaguzi ili kuwawezesha wale weye sifa waweze kuchaguliwa na hata kushiriki kuchagua wale wanaowataka.

"serikali itahakikisha inatekeleza wajibu wake wa kuhakikisha inatekeleza wajibu wake wa kusimamia katiba ili kila mwananchi mwenye sifa ya kuchagua au kuchaguliwa aweze kutekeleza haki yake ya kikatiba nila vikwazo vya aina yoyote”

Post a Comment

0 Comments