Kampuni ya
Mbolea Tanzania (TFC) imesaini Mkataba na Kampuni ya Sea Energy Group
Company ya Dubai tarehe 25 Juni 2025, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
mauziano ya mbolea aina ya UREA tani 23,000.
Mkurugenzi Mkuu wa
TFC, Bw. Samuel Mshote amesema kuwa lengo la TFC kwa mwaka wa fedha
2024/25 ilikuwa kusambaza mbolea ya ruzuku tani 100,000 na hadi sasa TFC
imesambaza tani 31,500 ya mbolea ya kupandia ya DAP, tani 35,000 za
mbolea ya kukuzia ya UREA N46% na tani 59,127 za mbolea kwaajili ya zao
la tumbaku.
Pia katika kupunguza gharama za uagizaji wa mbolea
TFC imeanza kujishughulisha na uwekezaji wa viwanda, kwa kuagiza mitambo
na kuifunga kwa ajili ya kuchanganya mbolea kulingana na aina ya
udongo.
Mbolea ya UREA N46% ni maalum kwa ajili ya kukuzia mazao
itauzwa kwa wakulima kwa bei ya ruzuku kwa utaratibu wa ruzuku ya
Serikali. Na itasambazwa kwa wakulima wote nchini.
Kwa upande
wake, Bw. Dean Tavakoli, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Sea
Energy Group Company ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya
Kilimo na kuahidi kuleta mbolea yenye viwango na gharama nafuu kwa
mkulima.
0 Comments