SHEIKH PONDA ACHUKUA FOMU YA UBUNGE TEMEKE

Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, Katibu wa Taasisi za Jumuiya za Kiislam Tanzania na Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo, Sheikh Ponda Issa Ponda amekabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Temeke.

 Sheikh Ponda amekabidhiwa fomu ya kugombea nafasi hiyo leo Juni 24, 2025 na Katibu wa ACT Wazalendo Jimbo la Temeke, Mussa Bakary, katika ofisi za jimbo iliyopo Kata ya Azimio, Tandika jijini Dar es Salaam.

Aidha, Sheikh Ponda amewahimiza wananchi kuchagua viongozi bora wanaofaa na watakaowasemea changamoto zao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika hatua nyingine, amewaasa wananchi kushiriki kikamilifu uchaguzi Mkuu 2025 na kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwani ni haki ya msingi ya kila mwananchi.

Post a Comment

0 Comments