NAIBU WAZIRI SANGU ATOA KONGOLE KWA PSSF

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu, ametembelea banda la PSSSF katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kitaifa, yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma na kuupongeza Mfuko kwa utoaji huduma bora kwa wanachama.

 “Ushiriki wenu umeonyesha dhamira yenu ya kuwahudumia watanzania naamini mmeweza kutoa elimu na hii ni moja ya mkakati wa kufikisha elimu kwa umma, hongereni sana.” Alisema.

Alisema kwa sasa Mfuko umekuwa ukifanya vizuri katika utekelezaji wa jukumu lake la msingi la ulipaji wa Mafao na hata Mfuko umeimarika kiukwasi.

“Niwapongeze kwa kuweza kuufanya Mfuko huu kuwa himilivu kwa maana ya kutekeleza vema jukumu la ulipaji wa mafao,” alisisitiza.

Aidha, ameomba Mfuko kuendelea kuimarisha ushirikiano baina yao na wz
aajiri.“Ili tuweze kwenda vizuri tuwapatie elimu wafanyakazi wanaokaribia kustaafu; Najua hili mnalifanya, lakini likifanyika miezi sita kabla itasaidia sana kuwawezesha watakapostaafu waweze kusimamia vema Mafao na zile pensheni za kila mwezi ili waweze kumudu maisha baada ya utumishi.” Alisema.

Post a Comment

0 Comments