RAIS SAMIA KUSHIRIKI UAPISHO WA RAIS HICHELEMA ZAMBIA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 01, 2026, anaondoka nchini kuelekea Lusaka, Zambia kuhudhuria sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Hakainde Hichilema. 

Katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika Agosti 13, 2026, Rais Hichilema alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano.

Ziara ya Rais Dkt. Samia inaendeleza uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Tanzania na Zambia, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda.

Post a Comment

0 Comments