RAIS SAMIA AONDOKA NCHINI AELEKEA ZAMBIA UAPISHO WA RAIS HICHELEMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kabla ya kuondoka nchini kuelekea Lusaka, Zambia.

Rais Samia anaelekea Zambia kuhudhuria Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema, kufuatia ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika Agosti 13, 2026.
 

Mhe. Hichilema amechaguliwa kuiongoza Zambia kwa muhula mwingine wa miaka mitano, katika uchaguzi uliowakutanisha wagombea mbalimbali kuwania nafasi ya Urais wa nchi hiyo.
 

Ushiriki wa Rais Samia katika hafla hiyo unaendelea kuakisi uhusiano wa kidiplomasia na wa kindugu uliopo kati ya Tanzania na Zambia, pamoja na ushirikiano wa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili.

Sherehe hizo za uapisho zinatarajiwa kufanyika Lusaka, Zambia, tarehe 1 Septemba 2026, ambapo viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Zambia wanatarajiwa kuhudhuria.



Post a Comment

0 Comments