Mkazi wa Kitongoji cha Katabradik, Kata ya Dareda wilayani Babati, Mkoa wa Manyara, Emmanuel Qamara, anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 65 na 70, anadaiwa kufariki dunia baada ya kushambuliwa na fisi.
GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA CHUMBANI NA VIKSI LOTION.
Tukio hilo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia leo, Jumatatu Agosti 31, 2026, ambapo baadhi ya mabaki ya mwili wa marehemu yamekutwa katika eneo lililo karibu na Shule ya Msingi St. Patrick Winters.
Baada ya tukio hilo, wananchi wameendelea na msako katika maeneo yanayozunguka eneo la tukio kwa lengo la kutafuta mabaki mengine ya mwili. Miongoni mwa vitu vilivyopatikana ni pamoja na viganja vya mikono, kitambulisho cha NIDA, simu ya mkononi, koti pamoja na rungu, ambavyo vimesaidia katika utambuzi wa marehemu.
Tukio hilo linadaiwa kuwa ni la tatu kuripotiwa katika eneo hilo, hali inayoongeza hofu miongoni mwa wananchi kutokana na uwepo wa fisi na ongezeko la mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na wanyama hao.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Seloto, Daniel Wema Duwe, amesema mashambulizi ya fisi yameongezeka mwaka huu na kwamba uongozi wa eneo hilo tayari umewasilisha taarifa kwa mamlaka zinazohusika na usimamizi wa wanyamapori.
Duwe amezitaka mamlaka kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo, huku wananchi wakitakiwa kuwa waangalifu na kuepuka kutembea katika maeneo hatarishi nyakati za usiku, wakati juhudi za mamlaka na wananchi za kukabiliana na tishio hilo zikiendelea.

0 Comments