WEZI SUGU WA MITA ZA MAJI WAKAMATWA-MOSHI

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linawashikilia watu wawili ambao ni Sharif Abdallah Mabishi (20) na Boniface Machila (22), raia wa nchi jirani, kwa tuhuma za wizi wa mita 14 za maji zinazomilikiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).

JE,HUPATI WATEJA? TANGAZA NASI KWA ELFU 5 UFIKE MAELFU  PIGA SASA 0654414804.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, Agosti 22, 2026, katika Kitongoji cha Miembeni, Kata ya Makuyuni, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Himo, Mkoani Kilimanjaro ambapo Askari Polisi kwa ushirikiano wa Wananchi na viongozi wa Serikali za Mtaa walibaini uwepo wa wanaume watatu katika eneo hilo majira ya saa 8 usiku, wakiwa na mita hizo kwenye pikipiki aina ya TVS yenye namba za usajili KMGW 960. 

 

Katika hatua hiyo, watu wawili walikamatwa, huku mmoja alifanikiwa kukimbia na kutokomea kusikojulikana na msako unaendelea ili kufanikisha kukamatwa kwake.

Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na baada ya kukamilika, hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linatoa wito kwa Wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kuwakata wahusika wa wizi wa mali za Serikali na uhalifu mwingine ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Post a Comment

0 Comments