MSAKO MKALI WABAINI BIASHARA YA NGONO ZEMBE-PEMBA

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Zuhura Mgeni Othman, amefanya ukaguzi katika nyumba iliyopo Chanjamjawiri, Pemba, inayodaiwa kutumika kwa shughuli za biashara ya ngono.

Katika ukaguzi huo, zimeonekana kondomu zinazodaiwa kuhusishwa na shughuli hizo, huku Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuna viashiria vinavyoashiria uwepo wa biashara ya kuuza mwili katika nyumba hiyo.

Zuhura amesema hali hiyo inatia wasiwasi kutokana na madai kuwa eneo hilo hutembelewa pia na vijana na watoto, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia vitendo vinavyokiuka maadili ya jamii.

Amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya dola wanapobaini maeneo yanayodaiwa kutumika kwa shughuli hatarishi, huku akisema hatua za kisheria zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.



Post a Comment

0 Comments