WAWILI WAHUKUMIWA JELA KWA KULAWITI

 Mahakama ya Wilaya ya Chunya imewahukumu watu wawili kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya ubakaji na ulawiti yaliyotokea maeneo tofauti wilayani humo.

GUSA HAPA,REJESHA HESHIMA CHUMBANI NA KAMA UNAHITAJI AJIRA SASA  

Amos Masanja (28), mkazi wa Igangwe, amehukumiwa miaka 30 jela kwa kumlawiti kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 20, tukio lililotokea Julai 7, 2026 katika Kijiji cha Igangwe.


Hukumu hiyo imetolewa Agosti 13, 2026 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Chunya, Bruno Bungole, baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi uliowasilishwa.

Katika tukio lingine, Lusekelo Kajingili (43), mkazi wa Chalangwa na baba wa kambo wa mwathirika, amehukumiwa miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumbaka mtoto wa miaka 15, mwanafunzi wa shule ya msingi.

Post a Comment

0 Comments